None
SW
IAEA, TAEC kusafirisha mabaki vyanzo vya mionzi
['Na Aveline Kitomary']
HabariLeo
DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), kwa kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), wamekubaliana na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kuanza mchakato wa kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake katika mashine za kutibu saratani.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mabaki ya vyanzo hivyo vya mionzi yatasafirishwa kwenda Hungary kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa mchakato wa kuyahuisha kwa matumizi mengine, kwa kuzingatia taratibu na viwango vya usalama vinavyotumika katika usimamizi wa vyanzo vya mionzi.
Mchakato wa kuondoa na kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi ni sehemu ya taratibu za kawaida za usimamizi wa vyanzo hivyo, zinazotekelezwa kwa ushirikiano wa mamlaka husika za ndani, TAEC na IAEA.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mabaki ya vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi yake yanadhibitiwa na kusimamiwa kwa usalama, huku vyanzo vipya vikiendelea kutumika katika kutoa huduma za tiba ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani.
Hatua hiyo pia inaashiria kuendelea kwa ushirikiano kati ya Tanzania na IAEA katika kuimarisha usalama wa matumizi na usimamizi wa teknolojia ya nyuklia katika sekta ya afya.