BUKOBA, KAGERA: Kampuni ya Helios Towers imezindua rasmi maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Shule ya Sekondari Katale iliyopo wilaya Bukoba mkoani Kagera, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kurudisha fadhila kwa jamii kupitia uwekezaji katika sekta ya elimu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania. Mradi huo umefadhiliwa na …