PWANI: JESHI la Polisi Mkoani Pwani limemebaini baadhi ya wanafunzi walioshindwa kuripoti shuleni kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro ya kifamilia. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcase, amesema kuwa hayo yamebainika mwezi Julai kutokana na mpango kazi wa kufuatilia wanafunzi ambao hawajaripoti …