BUKOBA: Waziri wa Maliasili na Utalii, Ashatu Kijaji, leo amekagua miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne mkoani Kagera. Katika ziara hiyo, Waziri amekagua miradi mitatu yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 23.8, ikiwemo ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Kyakailabwa, Soko Kuu la Bukoba …