MBEYA: Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imetembelea mradi wa uzalishaji wa kahawa wa Utengule Coffee Estate uliopo mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kufuatilia maendeleo ya miradi ya uwekezaji na kuhamasisha uwekezaji wenye tija unaochangia maendeleo ya uchumi wa taifa. Kwa sasa, mradi huo unazalisha takribani tani 200 …